Na Munir Shemweta, MLELE

Mkazi wa kijiji cha Luchima katika kata ya Majimoto halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile ametoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi.

Kiasi hicho cha pesa kimekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda tarehe 3 Mei 2024 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Luchima alipokwenda kuzungumza nao wakati wa ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko katika jimbo lake la Kavuu.

‘’Nampongeza rais kwa vitendo kabisa naomba mhe, mbunge leo nikikabidhiwa fedha taslimu shilingi elfu tano umpelelekee Mhe, Rais ’’ alisema.

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, uamuzi wake unatokana na kuwiwa na uongozi bora na utendaji kazi wa Rais Samia hasa kwa kuwajali wananchi wa Luchima ambapo mbali na mambo mengine amewajali kwa kutoa fedha milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati aliyoieleza imewakomboa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda amesema atahakikisha kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na mwananchi huyo kinamfikia mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amempongeza mwananchi huyo wa kijiji cha Luchima wa uamuzi wake wa kutoa kiasi hicho cha fedha kama ishara ya kukubali juhudi na kazi kubwa inayofanywa na Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Luchima na Tanzania kwa ujumla.

Amewaaleleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, Rais Samia anawapenda sana na amekuwa akisaidia juhudi mbalimbali za maendeleo kwenye jimbo la Kavuu na kutaja baadhi ya juhudi hizo kuwa ni pamoja na kutoa fedha za ujenzi wa hospitali, shule, barabara pamoja na upatikanaji wa huduma za maji.

Mhe, Pinda amefanya ziara katika jimbo lake la Kavuu kuwafariji wananchi waliopatwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa na kuathiri miundiombinu ikiwemo madaraja.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.
Mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile akizungumza mara baada ya kumkabidhi shilingi elfu tano Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda aliyoitoa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 3 Mei 2024.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya  Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akimpongeza mkazi wa kijiji cha Luchima katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi Bw. Aseni Jandikile aliyetoa shilingi elfu tano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za kuwaletea maendeleo wananchi tarehe 2 Mei 2024.

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu uwepo wa kimbunga “HIDAYA” katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya nchi yetu.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ilisema Kimbunga “HIDAYA” kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo hadi kufika saa tisa usiku wa tarehe 03 Mei 2024 kilikuwa kimeimarika zaidina kufikia hadhi ya Kimbunga kamili kikiwa umbali wa takriban Kilomita 401 mashariki mwa pwani ya Mtwara.

Aidha taarifa hiyo ilisema tangu wakati huo,kimbunga HIDAYA kimeendelea kuimarika zaidi huku kasi ya upepo ikiongezeka hadi kufikia
Kilomita 130 kwa saa. 


TASAC inawataarifu wadau wote wa usafiri kwa njia ya maji kuwa mwenendo wa mifumo  ya hali ya hewa baharini bado unaonesha uwezekano mkubwa wa Kimbunga “HIDAYA”  kusalia katika hadhi ya Kimbunga kamili kwa saa 12 zijazo huku kikiimarika, na kendelea kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania.

Hata hivyo taarifa ilisema Kimbunga hikikinatarajiwa kuendelea kuwepo hadi tarehe 06 mwezi Mei 2024 na kupungua nguvu baada ya tarehe 6 Mei 2024.

Uwepo wa kimbunga hicho utasababisha ongezeko la mvua na upepo mkali utakaoambatana na mawimbi makubwa baharini yatakayosambaa katika eneo kubwa la mwambao wa bahari yetu.

Kwa msingi huo, TASAC inatoa wito kwa wadau wote wanaofanya shughuli za kiuchumi, wakiwemo wavuvi,kuchukua tahadhari na kujiepusha kufanya shughuli hizo baharini hadi hapo kimbunga kitakapopita katika mwambao wa bahari yetu. 

Kwa vyombo vinavyofanya shughuli za usafirishaji abiria,tunawaasa kuchukua tahadhari kubwa na kutumia taarifa
za hali ya hewa kabla ya kuanza safari.

Aidha TASAC imewaasa wananchi kwa ujumla kujiepusha na shughuli za starehe katika mwambao wa bahari hadi hapo kimbunga kitakapopita katika mwambao wa bahari yetu.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Haki, weledi na uadilifu na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika.

Mhe. Sillo amesema hayo wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Jijini Dodoma na kuzungumza na Makamisha na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi ikiwa ni mara ya kwanza kutembelea Jeshi la Polisi tangu alipoteuliwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Aprili 4,2024.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeendelea kutekeleza makujukumu yake kwa weledi na uadilifu katika kuhakikisha shughuli za kila siku za Jeshi hilo zinaendelea kufanyika kwa kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wananchi.






Mawaziri wanaosimamia Sekta ya Afya katika Nchi Wanachama wa Jumuiya Afrika Mashariki wameweka mikakati na kukubaliana kuongeza ushirikiano zaidi katika kuboresha utoaji wa huduma katika sekta hiyo.

Azma hiyo imefikiwa leo tarehe 3 Mei 2024 kwenye Mkutano wa Kawaida wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya la Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Mawaziri hao wamekutana kwa lengo la kufanya mapitio na maboresho ya mikakati itakayosaidia kutatua chanagamoto zinazo changia kuzorota kwa ustawi wa sekta ya afya katika Jumuiya.

Sambamba na kufikia azima hiyo Mawaziri hao wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha mifumo na miundombinu ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo uimarishaji wa maabara, maboresho ya programu mbalimbali za afya, maboresho ya mafunzo kwa wataalam wa afya, maboresha ya sera za afya, utafiti na ufuatiliaji.

Vilevile wamejadili na kuweka mikakati makususi ya kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na shinikizo la juu la damu. Mikakati hiyo ni pamoja na kuwashauri na kuwahamasisha wananchi uzingatiaji wa mlo kamili, ufanyaji mazoezi na kuacha au kupunguza matumizi wa pombe.\

Akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Afya nchini Mhe. Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Tanzania inaendelea na utekelezaji wa mikakati hiyo, ambapo amebainisha kuwa katika suala la uhamasishaji wa ufanyaji mazoezi Serikali imechukua hatua ya kufunga daraja la Tanzanite la jijini Dar es Salaam kwa kila Jumamosi ili kuruhusu wananchi wa kufanya mazoezi katika daraja hilo.

Vilevile Waziri Ummy ametoa wito kwa Baraza hilo kukubali na kupitisha endekezo la Tanzania la kuanzisha Kituo cha Umahiri cha Upandikizaji Uloto (kwa wototo wenye sickle Cell) na Sayansi ya Matibabu ya Magonjwa ya Damu chini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa na Kituo cha Umahiri cha Sayansi ya Afya ya Kinywa chini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)

Mbali na hayo Mawaziri hao wamejadili kuhusu namna ya kubaliana na changamoto mbalimbali zinazochangia kuzorota kwa sekta hiyo katika Jumuiya. Wamezita changamoto hizo kuwa ni pamoja na Mabaliko ya Tabia Nchi, uhaba wa fedha za kuendesha programu na miradi mbalimbali ya afya, milipuko ya magonjwa, kuzuka kwa vita na mapigano kwenye baadhi ya maeneo katika Jumuiya, uhaba wa wataalam na miundombinu isiyotosheleza mahitaji ikiwemo vituo vya afya na vifaa tiba.

Katika kukabiliana na changamoto hizo wamepitisha mikakati kadhaa ya kukabiliana nazo ikiwemo; kupishwa ni kuimarisha mfumo wa ununuzi wa dawa kwa pamoja, kupitisha mpango mkakati wa pamoja wa masuala ya afya wa Jumuiya kwa mwaka 2024 hadi 30, kuimarisha ufuatiliaji na utambuzi wa wagonjwa, kukamilisha na kuwasilisha andiko la kuomba fedha za kukabiliana na majanga, kuimarisha afua za kinga ili kutokomeza malaria katika Jumuiya na kuendelea kusimamia Vyuo Vikuu vya Afya ili viendelee kutoa elimu bora ndani ya Jumuiya.

Mkutano huo uliofanyika kwa siku tano kuanzia terehe 29 Aprili hadi tarehe 3 Mei 2024 uliaanza katika Ngazi ya Wataalam ambapo pamoja na masuala mengine walikufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano wa 23 wa Baraza hilo. Tarehe 2 Aprili 2024 uliendelea katika Ngazi ya Makatibu Wakuu na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri tarehe 3 Mei 2024.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akichangia mada kwenye Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.
Mawaziri na Makatibu Wakuu wanaosimamia Sekta ya Afya katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mei 3, 2024.
Mkutano wa 24 wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Afya wa Afrika Mashariki ukiendelea.

IJUMAA ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet tayari wamekuwekea ODDDS za kibabe na machaguo zaidi ya 1000. Ingia meridianbet na usuke mkeka wako hapa.

EPL leo hii kutakuwa na mechi moja ambayo Luton Town atakuwa mwenyeji wa Everton ambao wametoka kushinda mechi yao iliyopita. Mwenyeji anahitaji pointi tatu leo ili ajiweke kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi. Meridianbet wamempa The Toffees nafasi kubwa ya kushinda mechi hii kwa ODDS 2.55 kwa 2.60. Beti sasa.

Ligi kuu nyingine ambayo leo hii itaendelea ni kule Hispania yaani LALIGA mechi moja ya Getafe dhidi ya Athletic Club ambao wapo nafasi ya tano kwenye ligi. Mechi hiyo itapigwa kwenye dimba la Coliseum huku mechi ya mwisho walipokurtana walitoshana nguvu. Mechi hii imepewa ODDS 3.57 kwa 2.16. Jisajili hapa.

Ukiachana na mechi ndugu mteja kumbuka kucheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni ambayo inatolewa ndani ya meridianbet kama vile Poker, Roullette, Aviator, Rockertman, Keno, Sloti na mingine kibao. Ingia mchezoni na ucheze sasa.

Lakini vilevile BUNDESLIGA nayo itarindima ambapo RB Leipzig baada ya kushinda mechi yake iliyopita, leo hii atakuwa ugenini kusaka pointi tatu dhidi ya TSG Hoffenheim. Mwenyeji ametoka kupoteza mchezo wake uliopita huku ndani ya Meridianbet anayependelewa zaidi kuondoka na pointi tatu ni RB akiwa na ODDS 1.47 kwa 5.48.

Halikadhalika SERIE A leo hii itakuwa mzigoni saa 3:45 Torino atapepetana dhidi ya Bologna ambao wamekuwa na kiwango kizuri sana msimu huu. Mwenyeji yupo nafasi ya 10 na mgeni yupo nafasi ya 4. Tofauti ya pointi kati yao ni 17. Je nani kuibuka kidedea? Bashiri mechi hii sasa. Ikiwa imepewa ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000.

LIGUE 1 kule Ufaransa kuna mechi ya kibabe kabisa Toulouse uso kwa uso dhidi ya Montpellier ambao wametoka kutoa sare mechi yao iliyopita. Mwenyeji yeye aliondoka na ushindi. Mechi ya mkondo wa kwanza kukutana, Mgeni alishinda. Je leo hii Toulouse atalipa kisasi?. Beti mechi hii sasa.

Mechi nyingine itakuwa majira ya saa 4:00 usiku ambapo RC Lens baada ya kupoteza mechi iliyopita, leo atakuwa nyumbani kuzichabanga dhidi ya FC Lorient ambao wapo nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye ligi. Meridianbet wamempa mwenyeji nafasi ya kushinda kwa ODDS 1.39 kwa 7.05. Nani kushinda leo huku mechi ya kwanza walipokutana walitoshana nguvu.?
--Awahimiza Wachungaji kuwa na Maono Makubwa
--Awataka kuhubiri amani na upendo
--Awahimiza kumtia moyo Rais Samia kutekeleza miradi ya maendeleo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewashauri wachungaji kuwa na maono makubwa katika kuongoza waumini katika makanisa yao ili kujenga Taifa la watu wenye mwelekeo chanya.

Akizungumza leo (Mei 3, 2024) Jijini Dodoma wakati wa kufunga kikao cha mazungativu (Retreat) kwa wachungaji wa Kanisa la FPCT, Dkt. Biteko amesema kuwa ili waumini wapate uelekeo wa kwenda mahali fulani, wanahitaji mtu mmoja miongoni mwao atakaye waongoza kufikia malengo waliyojiwekea kutokana na maono aliyonayo.

“Wachungaji msihangaike na wingi wa watu mahali popote, angalia uwezo wa kiongozi anayeona mbali atawaongoza wafike mbali”, amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa “ Askofu Mkuu umechagua fungu jema kufanya wachungaji hawa wakutane hapa kujiongezea maarifa kwa kuwa tuko katika dunia iliyojaa utandawazi na mafundisho ya kweli na yasiyo ya kweli. Ni vigumu kwa waumini kutambua ya kweli na yasiyo ya kweli hivyo, wanahitaji kuongozwa”.

Aidha, Dkt. Biteko amewahimiza viongozi wa dini kuwaongoza waumini kiroho na kuchagua viongozi sahihi wanaofahamu kuwa watawaletea maendeleo na ustawi wa nchi.

Pia, amewaomba viongozi wa dini kuwahimiza waumini kufanya kazi kwa bidii, kuhubiri kuhusu amani pamoja na kusisitiza maadili kwa waumini.

Dkt. Biteko ametaja mafanikio mbalimbali ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, huku akiwaomba wachungaji hao kuendelea kumuombea na kumtia moyo ili aendelee kutekeleza miradi ya nchi katika maeneo mbalimbali.

“ Mradi wa reli ya kisasa (SGR) ni mradi mkubwa haikuwa rahisi kupata fedha za kutekeleza mradi huu lakini Rais Samia amefanikiwa, Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere unaozalisha megawati 2115 umefanikiwa, Pia Serikali imejenga madarasa, zahanati, vituo vya afya na kutoa ajira kwa watumishi wa sekta ya afya, angalieni nia yake, muungeni mkono”, amebainisha Dkt. Biteko.

Vilevile, amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa dini na imani za watu hivyo viongozi wa dini wahimize waumini kuchagua viongozi wanaofaa

“Mwaka huu tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa dini mna uwezo wa kuwahamasisha waumini waweze kuchagua viongozi wanaowahitaji kwa ajili ya kuwaletea maendeleo”, amesisitiza Dkt. Biteko.

Naye, Askofu Mkuu wa FPCT, Steven Mulenga amesema kuwa lengo la semina hiyo ya siku nne kwa wachungaji ni kuwajengea uwezo watumishi wa Mungu namna ya kumkaribisha Yesu Kristo.

“ Haya tuliyofundishana yatakuwa na matokeo kwa nchi ya Tanzania”, amesema Askofu Mulenga.

Semina hiyo wa wachungaji FPCT imehudhuriwa na wachungaji kutoka nchi za Kenya, DRC, Rwanda na Sudani Kusini.






NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabishara wa bidhaa za vipodozi kuhakikisha wanasajili bidhaa zao , kuthibitisha ubora wake pamoja na kusajili maeneo yanayohusika na uzalishaji, uuzaji na uhifadhi kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya viwango Sura ya 130 ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.

Wito huo umetolewa leo Mei 3, 2024 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya wakati akifungua Kikao baina ya TBS na wazalishaji, waagizaji na wasambazaji wa bidhaa za vipodozi nchini.

"Madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu ni pamoja na saratani ya ngozi, kuathiri mfumo wa uzazi, kuathiri figo, kuathiri afya ya ngozi na kusababisha ngozi kushindwa kuhimili joto pamoja na kushambuliwa kirahisi na magonjwa ya ngozi". Amesema Dkt. Ngenya.

Aidha Dkt. Ngenya amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023 hadi mwezi Aprili 2024, wamekamata na kuharibu vipodozi vyenye viambata sumu vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa tani 114 na thamani ya shilingi bilioni 1.49.

Amesema kuwa Shirika litaendelea kuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wale watakaoendelea kukiuka matakwa ya sheria katika uuzaji wa vipodozi.

Amesema wafanyabiashara hao wa vipodozi wanapaswa kuhakikisha wanazalisha na kusambaza bidhaa za vipodozi vilivyokidhi matakwa vya viwango ili visiweze kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa bidhaa hizo.










Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, amesema kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan, ndiyo siri na chachu ya chama na viongozi wake katika kuwatumikia wananchi.

Balozi Dk Nchimbi ameongeza kusema kuwa katika kutekeleza kwa vitendo Falsafa ya 4R ya Mhe. Rais Samia na kuwatumikia wananchi waliokipatia dhamana ya kuongoza, CCM kikiwa Chama kiongozi nchini, kitaendelea kutimiza wajibu wake wa kuwaunganisha Watanzania kuwa wamoja wenye mshikamano bila kubaguana kwa kuangalia maeneo wanayotoka, dini, kabila wala itikadi za kisiasa.

Balozi Dkt Nchimbi, ameyasema hayo wakati wa mazungumzo kati yake na Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha Burundi, CNDD РFDD, Mhe. R̩v̩rien Ndikuriyo, yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam, leo Ijumaa, Mei 3, 2024.

“Asante kwa pongezi zako za utekelezaji wa ilani ya CCM. Mojawapo ya nguzo za uimara wa CCM ni pamoja na kazi kubwa sana zilizofanywa na Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya miaka hii mitatu. Zinatupatia ujasiri na jeuri ya kuwa barabarani, kwenda kuzungumza na wananchi kwa sababu tunayo mambo ya kusema na kuonesha. Na wananchi wanatuunga mkono.

“Lakini pia katika uhusiano kati yetu, CCM tunafurahi sana jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Burundi, Mheshimiwa Évariste Ndayishimiye ni marafiki. Hivyo vyama vyetu ni marafiki, nchi zetu ni rafiki na hata viongozi wetu ni marafiki, ni wajibu wetu sisi tuendelee kuenzi na kulinda uhusiano na ujirani wetu mwema, kwa ajili ya watu wetu wa pande zote mbili,” amesema Balozi Dk Nchimbi.

Kwa upande wake Mhe. Ndikuriyo amesema kuwa CCM na Tanzania kwa ujumla, ni sehemu muhimu kujifunza kwa ajili ya kujiimarisha, hususani wakati huu ambapo Chama cha CNDD – FDD kinaendelea kuisimamia Serikali ya Burundi katika kulinda misingi ya demokrasia inayotokana na utashi wa Warundi.

Katika ujumbe wake, Mhe. Ndikuriyo aliambatana na
Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Mhe. Leontine Nzeyimana na maofisa wengine wa Chama cha CNDD - FDD kutoka Burundi.



Na Munir Shemweta, MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda amekabidhi baiskeli za walemavu wa miguu ikiwa ni jitihada za kuwasaidia watu wenye ulemau.

Mhe, Pinda amekabidhi baiskali tarehe 2 Mei 2024 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kirida katika Kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi.

Baiskeli iliyokabidhiwa kwa mlemavu Bi. Adela John mkazi wa Kirida ni sehemu ya baiskeli nne zilizotolewa kwa walemavu wa miguu wa jimbo la Kavuu ikiwa ni njia ya kuwasaidia usafiri wa kuwawezesha kwenda maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hiyo, Mbunge wa jimbo hilo na Naibu Waziri wa Ardhi Mhe, Pinda amesema kuwa, anatambua adha wanayoipata walemavu wa miguu katika jimbo lake ndiyo maana ameona ipo haja ya kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kwenda katika shughuli zao.

‘’Ni matumaini yangu kuwa baiskeli hii itakuondolea adha uliyokuwa ukiipata na kwa sasa itakusaidia sana wakati wa kwenda katika shughuli zao mbalimbali’’ alisema Mhe, Pinda.

Mapema kwenye mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele mkoa wa Katavi, Mhe, Pinda aliwaeleza wananchi wa kijiji hicho kuwa, pamoja na kukabiliwa na majukumu ya uwaziri lakini amekuwa akifanya juhudi ya kuwatumikia katika kuwaletea maendeleo.

Amezitaja juhudi hizo kuwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, zahanati na vituo vya afya, madaraja na shule za msingi na sekondari sambamba na upatikanaji huduma za umeme na maji.

‘’Pamoja na kwamba hamnioni mara kwa mara nikija hapa Kirida kutokana na majukumu niliyo nayo lakini nimekuwa nikifanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo na haya maendeleo mnayo yaona kama vile ujenzi wa bararbara, shule, zahanati na vituo vya afya, zote ni jitihada ambazo ninazifanya’’. Alisema Mhe, Pinda.

Awali wananchi wa Kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba walimueleza mbunge wa jimbo hilo kuwa wanakabiliwa na changamoto malimbali ikiwemo kutofanyika vikao vya kijiji kwa ajili ya kujua mapato na matumizi, kuwekewa alama za mipaka maeneo ya nyumba zao kwa madai kuwa makazi hayo yapo kwenye kingo ya mto na hivyo kutakiwa kuhama wakati mto ndiyo umehama.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda (Kushoto) akimkabidhi Baiskeli Mlemavu wa Miguu Bi. Adela John wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kidira katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mei 2, 2024. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi Mhe, Geophrey Pinda na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe Silas Ilumba wakimuangalia Bi. Adela John ambaye ni mlemavu wa miguu mara baada ya kumkabidhi baiskeli tarehe 2 Mei 2024.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakati wa ziara yake katika jimbo la Kavuu Mei 2, 2024.
Beda Andrea mkazi wa kijiji cha Kirida Kona akiwasilisha changamoto zake kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kirida kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe Mei 2, 2024.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kirida katika kata ya Mamba halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe, Geophrey Pinda (Hayupo pichani) wakati wa mkutano wa hadahara uliofanyika kijiji cha Kirida Mei 2, 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji wa Serikali waondoe ukiritimba kwenye suala la upatikanaji wa habari ili kuwawezesha wanahabari kupata taarifa sahihi na kufanya kazi zao kwa ufanisi.

“Viongozi na Watendaji wa Serikali na Mashirika zingatieni Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa ya Mwaka 2016 na ondoeni ukiritimba katika suala la upatikanaji wa habari ili wanahabari wawezeshwe kupata taarifa sahihi na wafanye kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu,” amesema.

Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Mei 3, 2024) wakati akizungumza na wanahabari na wadau wengine kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Kuhusu upatikanaji wa habari sahihi, Waziri Mkuu pia amewataka wakuu wa taasisi waweke mazingira mazuri kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha kuzingatia weledi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa ngazi zote za jamii.

Aidha, amevitaka vyombo vya habari viunde madawati maalum yatakayoratibu masuala ya mabadiliko ya tabianchi. “Madawati hayo yatafute fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango wa mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu kuandika kitaalamu masuala ya mabadiliko ya tabianchi na madhara yake kwa jamii na Taifa. Suala hili likamilike ili katika maadhimisho ya siku hii mwakani, iwepo taarifa ya utekelezaji,” amesisitiza.

Kuhusu habari za uchunguzi, Waziri Mkuu amesema uandishi wa habari hizo unahitaji rasilimali fedha za kutosha ili kutoa mafunzo na kuifanya kazi yenyewe. “Niwaombe wadau wote muhimu wakiwemo taasisi, asasi za kiraia na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi washirikiane na vyombo vya habari katika kufanikisha utafiti na uandishi wa habari za uchunguzi na kuvisaidia vyombo vya habari kukua kitaaluma na kiuchumi.”

Akigusia changamoto zinazowakabili waandishi wa habari wanawake, Waziri Mkuu amezitaka Wizara za Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na ile ya Maendeleo ya Jamii Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, zihakikishe zinakamilisha awamu ya pili ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (NPA-VAWC II). “Hatua hiyo itasaidia ushughulikiaji wa changamoto za mashambulio ya kimwili kwa waandishi wa habari wanawake,” amesema.

Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wanahabari wote wazingatie uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi kwa kutoa mchango chanya kwa jamii kwani wasipofanya hivyo tasnia hiyo inaweza kuwa chanzo cha kufifisha maendeleo na hata kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema vyombo vya habari vinayo nafasi kubwa ya kuitangaza nchi pamoja na kuijengea taswira chanya kimataifa na kuwapomgeza wanahabari kwa kazi wanayoifanya ya kuuhabarisha umma.

“Vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa katika kuhamasisha uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii na kuchangia katika kuinua uchumi wa Taifa letu. Kwa niaba ya Serikali na wananchi wote wa Tanzania ninavipongeza sana vyombo vyetu ya habari kwa kazi kubwa inayofanywa katika kuutumikia umma.”

Akisisitiza umuhimu wa vyombo hivyo, Waziri Mkuu amesema vina mchango mkubwa wa kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika shughuli na utekelezaji wa mipango ya Serikali pamoja na kampeni muhimu za kitaifa.

“Waandishi wa habari wana nguvu ya kuongeza sauti kwa jamii kuhusu mmomonyoko wa maadili, athari za kimazingira, kufichua rushwa na uzembe na kuunga mkono masuluhisho yatakayochochea maendeleo endelevu na ustahimilivu katika maeneo muhimu.

Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani kwa mwaka 2024 inasema: “Uandishi wa Habari na Changamoto za Mabadiliko ya Tabianchi.”

Mapema, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imeimarika ikilinganishwa na ilivyokuwa awali.

“Hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini inaendedelea kuimarika. Bado hatujafika tunakotaka kwenda lakini kwa hakika hatupo tulipokuwa jana. Tumefika hapa kutokana na juhudi za Mheshimiwa Rais, tumetekeleza 4R za Mheshimiwa Rais na ndiyo maana tuko hapa tulipo,” alisema.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo mabalozi wa Marekani, Uswisi, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, UNESCO, Asasi za Kiraia, Wawakilishi kutoka Muungano wa Klabu 28 za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Jukwaa la Wahariri na wanavyuo.




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Mei 3, 2024 amekutana na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taasisi ya Huduma za Aga Khan, Mwana wa Mfalme Bi. Zahra Aga Khan na ujumbe wake, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Mheshimiwa Waziri Mkuu amemwambia Kiongozi huyo kuwa Serikali inatambua jitihada kubwa zinazofanywa na Taasisi hiyo hasa katika sekta ya Afya na Elimu na amemuahidi kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za uwekezaji zinazofanywa na Taasisi ya hiyo.



Top News